Henri II
Mtakatifu Henri II (6 Mei 972 – 13 Julai 1024), alikuwa kaisari wa Dola Takatifu la Kiroma tangu tarehe 7 Juni 1002 hadi tarehe 13 Julai 1024.
Ni kaisari pekee wa Ujerumani aliyetangazwa kuwa mtakatifu. Ilitokea mnamo Julai 1147 kwa tamko la Papa Klementi II.
Sikukuu yake ni tarehe 13 Julai[1].
Ndoa yake na maisha ya kiroho
[hariri | hariri chanzo]Mke wake, Kunegunda wa Luxemburg, akaja pia kutangazwa mtakatifu na Papa Inosenti III mwaka 1200. Ilisadikiwa kwamba hawakuzaa watoto kutokana na uamuzi wao wa kuishi katika ndoa kama kaka na dada kwa sababu za kidini[2].
Hakika Henri alijiunga kiroho na Wabenedikto kama mtawa wa nje.
Pamoja na mkewe alishughulikia sana ustawi wa Kanisa Katoliki katika dola lake kwa kutetea haki za maaskofu na kuhimiza uaminifu wa mapadri kwa useja mtakatifu uliowapasa. Vilevile alijitahidi kueneza imani ya Kikristo kote Ulaya. Kwa ari hiyo ya kimisionari alianzisha majimbo mengi na monasteri.
Angalia pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya Makaizari wa Ujerumani
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Catholic Encyclopedia: Henry II
- Charter given by Emperor Henry for Niederaltaich Abbey showing the Emperor's seal, 25.6.1011 . Taken from the collections of the Lichtbildarchiv älterer Originalurkunden Archived 13 Januari 2009 at the Wayback Machine. at Marburg University
- Henry II at Patron Saints Index
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Ujerumani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Henri II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |